KUHUSU TOVUTI HII

 

Utangulizi

Karibu kwenye tovuti yetu.

Kwanza tutoe shukrani zetu za dhati kwa uamuzi wako wa kuitembelea tovuti yetu, kwetu ni faraja kubwa sana kuwa nawe siku hii ya leo.

Hii ni tovuti  tuliyoiandaa kwa lengo moja kuu la kumwezesha mwananchi wa kawaida ambaye hawezi kuelewa maelezo yanayotolewa na tovuti nyingine zinazotoa maelezo kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya na dawa mbalimbali za kuondoa matatizo hayo  kwa lugha za kigeni. Lengo letu ni kumwezesha mwananchi wa kawaida kupata maelezo ya matatizo hayo na dawa hizo kwa lugha nyepesi ya kiswahili ili aweze kuelewa na kutoa maamuzi yaliyo sahihi.  Tunaamini watu wengi hushindwa kunufaika na tovuti mbalimbali kwa sababu ya kushindwa kuzielewa lugha zilitotumika katika tovuti hizo.

Kuna tovuti nyingi zinazolenga kumsaidia mteja kupata mahitaji yake ya kuboresha afya, kwa bahati mbaya nyingi hutumia lugha za kigeni hivyo kumfanya mtu anayetumia kiswahili pekee kushindwa kunufaika na maelezo hayo. Kwa kugundua pengo hilo, tumeamua kuanzisha tovuti hii.

Malengo Ya Tovuti

Kukusanya maelezo kwa kutumia wataalamu wetu wenye uzoefu wa biashara za kwenye mitandao ya dawa mbalimbali ambazo zimethibitika kusaidia watu wengi duniani na kuziorodhesha katika tovuti hii.

Kumsadia mwanachi ambaye atavutiwa na dawa aliyoisoma kuinunua nje ili aweze kuipata na kuitumia.

Kutoa fursa kwa watu wote wenye uzoefu katika fani hii na watumiaji wa dawa zilizoorodheshwa ndani ya tovuti hii kutoa michango yao ya mawazo kuhusu ubora wa dawa mbalimbali kwa kupitia blog yetu au sehemu ya comments chini ya kila ukurasa. Imani yetu ni kupata mawazo zaidi kuhusu ubora wa dawa tulizoziorodhesha humu na dawa nyingine ambazo hazijaorodheshwa hapa ambazo watu wengine wameshazitumia.

Mpangilio Wa Tovuti

Tovuti hii imepangwa kwa kutumia aina ya matatizo ambayo mtu anaweza kuwa nayo na anatafutia suluhisho. Kwa mfano, dawa zote zinazosaidia kupunguza uzito au unene ( weight loss products ) zitaorodheshwa pamoja na zile za kupunguza mwonekano wa kiumri ( anti-aging products ) zitaorodheshwa kwenye kundi moja hali kadhalika dawa za matatizo ya mifupa ( bone  and joint products ), dawa za  afya ya  mwanamke na dawa za afya ya viungo vya  uzazi vya mwanamme. Tumetenga sehemu nyingine kwa ajili ya matatizo ya afya mseto ambapo hapa tumejuimisha matatizo mengi yakiwemo matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa kisukari, vidonda vya tumbo (peptic ulcers), kiharusi (stroke), msongo wa mawazo (stress), mfadhaiko (depression), Pumu, UTI, Kansa, High Blood Pressure (Hypertension), UKIMWI, hernia, tezi dume, mkanda wa jeshi,  Chunusi, n.k.

 

Post a Comment

0 Comments