DAWA NA MATIBABU SAHIHI YA VIDONDA VYA TUMBO

 


UTANGULIZI

Miili yetu imeumbwa kutegemea vyanzo viwili vya nguvu: oksijeni na vyakula. Oksijeni huingizwa ndani ya miili yetu kupitia pumzi na moja kwa moja huingia katika utendaji, wakati chakula hutakiwa kupitia mchakato mrefu ili kuweza kutumiwa na mwili, muundo na mchakato huu huitwa mfumo wa usagaji chakula ambao ni tumbo (mfuko wa chakula), utumbo mdogo (au kwa jina jingine utumbo mwembamba), utumbo mpana (au kwa jina jingine utumbo mkubwa), kibofunyongo, ini na kongosho. Tatizo lolote katika viungo hivi huweza kusababisha mwili wote kuugua.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya watu milioni 6 duniani hufa kutokana na matatizo mbalimbali yanayotokana na mfumo wa viungo vya usagaji chakula. Vidonda vya tumbo ikiwa ni mojawapo ni mmomonyoko katika kunyanzi za tumbo, sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo (duodeni), au umio (koromeo), huua 4% ya watu duniani.
 
Kwa hakika, vidonda vya tumbo ni ugonjwa ambao sasa unawasumbua watu wengi kote duniani, hasa katika nchi zinazoendelea na Ufilipino ikiwa inaongoza.
 
Katika miaka ya nyuma, vidonda vya tumbo lilikuwa ni tatizo la watu wachache sana hususan watu wenye umri mkubwa takriban kuanzia miaka 50, na wafabiashara wakubwa kutokana na misongo mikali ya kibiashara na ulaji mwingi wa vyakula vya kuchachua.
 
Lakini kulingana na mtindo wa maisha wa zama hizi, vidonda vya tumbo limegeuka kuwa tatizo la wote vijana kwa wazee. Inakadiriwa kwamba kati ya 10% hadi 20% ya watu duniani, hupata vidonda vya tumbo walau mara moja katika maisha yao.
 
Tatizo ni kwamba, watu wengi hujikuta ugonjwa ukiwa mkubwa kutokana na kudharau dalili za awali kwa kuziona ni za kawaida; hivyo kutoshughulikia matibabu ipasavyo. Wengi wanafahamu kuwa vidonda vya tumbo vinaleta maumivu katika tumbo, lakini hawafahamu kama ugonjwa huu unaweza kuwa tishio la uhai.
 
Karibu mgonjwa mmoja wa vidonda vya tumbo vinavyotokea katika mfuko wa chakula (gastric ulcers) kati ya kila wa wagonjwa 20 huweza kupata saratani ya tumbo. Hata hivyo, vidonda vya tumbo vinaweza kutibiwa kabla havijazaa magonjwa mapya.

Post a Comment

0 Comments