Wanawake wengi hukutana na tatizo la kutokwa damu baada ya
kumaliza kufanya mapenzi. Ukweli ni kwamba karibu asilimia 63 ya wanawake
waliokoma hedhi hukumbana na matatizo ya ukavu kwenye uke na kutokwa damu baada
ya tendo la ndoa.
Kinachosababisha
Kutokwa damu baada ya Tendo la Ndoa.
Kutokwa damu baada ya tendo la ndoa inaweza kutokea kwa
mwanamke wa umri wowote. Kwa wanawake wadogo ambao bado hawajafikia kukoma
hedhi chanzo kikubwa cha tatizo ni kwenye mlango wa kizazi (cervix). Wanawake
walikoma hedhi, chanzo cha tatizo hutofautiana yaweza kuwa kwenye
Mlango wa kizazi
Kizazi
Kwenye mashavu ya uke na kwenye
Njia ya mkojo.
Maambukizi.
Maambukizi kwenye njia ya uzazi au mkojo yanaweza kupelekea
kutokwa damu baada ya tendo la ndoa. Maambukizi haya ni kama
PID
Magonjwa ya zinaa
Maambukizi kwenye uke na
Maambukizi kwenye mlango wa kizazi.
Genito-urinary Syndrome of Menopause (GSM)
Tatizo hili kwa kifupi GSM hutokea zaidi kwa wanawake
wanaokaribia kukoma hedhi, wale waliokoma hedhi na wanawake waliokwisha
kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mifuko ya mayai (ovari).
Wanawake wanapofikia ama kukaribia kukoma hedhi, kiwango cha
homoni ya estrogen hupungua. Estrogen inavopungua, baadhi ya dalili hutokea
kwenye uke wako.
Mwili huanza kuzalisha kiwango kidogo na maji maji yanayolainisha uke, na hivo kupelekea uke kuwa mkavu na kuvimba wakati mwingine. Kiwango kidogo cha estrogen hupelekea pia kupungua kwa hali ya kuvutika ya uke. Tishu za uke zinakuwa nyembamba na kusinyaa. Hali hii hupelekea maumivu kwenye tendo la ndoa, kukosa uhuru na pia kutokwa damu.
Ukavu kwenye Uke.
Uke kuwa mkavu ni sababu ingine ya kutokwa damu baada ya
tendo la ndoa kwa mwanamke. Uke mkavu unaweza kusababishwa ana vitu hivi.
Kunyonyesha
Upasuaji wa kuondoa
mifuko ya mayai
Matumizi ya dawa mfano za pumu, dawa za kupunguza athari ya
msongo wa mawazo.
Chemotherapy na radiotherapy
Kufanya ngono bila kuandaliwa
Matumizi ya kemikali na sabuni kwenye kuosha uke
Kulegea kwa Uke
Uke unaweza kulegea na kupata majeraha hasa mwanamke
akifanya ngono kupita kiasi pasipo mpangilio (rough sex). Majeraha hutokea
zaidi pale mwanmke anapokuwa amekoma hedhi au siku chache baada ya kujifungua.
Saratani
Kutokwa damu kusiko na mpangilio, hasa baada ya tendo la
ndoa ni moja ya dalili ya saratani ya shingo ya kizazi. Ni muhimu kuwahi kufika
hospitali kama tatizo litaendelea kuwa la muda mrefu.
Saratani ya shingo ya kizazi nuwapata zaidi wanawake wenye umri zaidi ya miaka 50 au waliokoma hedhi. sababu zingine hatarishi ukiachilia mbali umri ni pamoja na uzito mkubwa, matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi, na maambukizi ya virusi wa papiloma.
Maelezo ya mwisho
Kumbuka unahitaji kumwona daktari endapo unaona dalili kama
Muwasho ukeni au hali ya kuungua
Hali ya kuungua ukeni wakati wa kukojoa
Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
Hedhi nzito yenye mabongemabonge
Maumivu ya mgongo wa chini
Maumivu makali ya tumbo
Kutapika na kichefuchefu
Kutokwa na uchafu ukeni kusiko kawaida
Athari za Kutokwa Damu baada ya Tendo la Ndoa.
Upungufu wa damu (Anemia)
Kutokwa damu kwa muda mrefu hupelekea mwanamke kuishiwa damu. Kutokana na kupoteza chembechembe nyingi nyekundu za damu. Upungufu wa damu huambatana na dalili hizi
Mwili kukosa nguvu na ganzi
Uchovu mara kwa mara
Kupata hali ya kusinzia muda mwingine
Maumivu ya kichwa na
Kubadilika rangi ya ngozi
0 Comments