TUNATIBU UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA CHAKULA

 Ikiwa wagonjwa wangebadilisha kile wanachokula, basi wangeacha kabisa kutumia dawa za hospitali. Wagonjwa wa kisukari, moyo, maumivu ya viungo, maumivu ya tumbo, n.k; moja kwa moja ni matokeo ya lishe mbaya. Nimetibu wagonjwa wa kisukari cha Aina ya pili kwa chakula, ndani ya miezi 6 wengi wamepona na wengine kupata nafuu kubwa sana. Halikadhalika wagonjwa wa maumivu ya viungo sugu, wagonjwa waliokuwa wanahitaji upasuaji wa moyo au upasuaji wa mishipa ya miguu na wengi wamepona kwa tibalishe. Magonjwa mengi husababishwa na chakula kibaya na huponywa na chakula kizuri.

Chochote unachokula kina athari nzuri ama mbaya kwenye afya yako. Na jinsi ulivyo ni kutokana na chakula unachokula. Mathalani kama utakula chakula kilichosindikwa na kuongezewa sukari na chumvi, ndani ya muda mfupi utakumbwa ama na ugonjwa wa kisukari au ugonjwa wa moyo au vyote viwili n.k.

Virutubisho mbalimbali vilivyo kwenye vyakula vimetengenezwa na MWENYEZI MUNGU Mwumbaji kwa ajili ya kukulinda na magonjwa mbalimbali. Kinyume chake, ukikosa virutubisho hivyo, basi maradhi kwako ni kitu cha kufikia. Mathalani kutopata vitamid C ya kutosha, vitamini D na folate huweza kusababisha moyo wako kupata shida, kinga ya mwili kupungua, na baadhi ya saratani.  Wagonjwa wa saratani ya mapafu wanaokula kwa wingi vyakula vyenye  Vitamini D ni rahisi sana kupata nafuu kubwa na hata kupona kabisa kuliko wagonjwa wanaopata vitamin D kwa kiwango kidogo sana.

Katika Kliniki yetu Moro Herbal Clinic iliyoko jijini Mwanza, tunakuletea huduma bora kabisa na ya kipekee sana; ambapo TUNAKUTIBU tatizo la kupungua nguvu za kiume kwa chakula sahihi kulingana na tatizo lako na TUNAKUTIBU kwa dawa zetu za asili kulingana na sababu na chanzo cha tatizo lako. Mwungano wa chakula na dawa sahihi za asili hufanya kazi vizuri sana na kwa haraka sana katika kutibu na kumaliza kabisa tatizo la kupungua kwa nguvu za kiume.

Usikupruke kubugia dawa za nguvu za kiume pindi unapoona una tatizo. Ni kosa kubwa mnoo! Upungufu wa nguvu za kiume hautibiwi kwa dawa moja unawapa watu wote. Au kwa aina moja ya chakula ambacho ati kila mtu unamshauri chakula hicho hicho! Kila mtu na dawa yake na kila mtu na chakula chake. Mathalani huyu kapungukiwa nguvu za kiume kwa sababu homoni ya testpsteroni iko chini sana, lakini mwingine kwa sababu homoni hiyo hiyo iko juu sana. Au huyu kapungukiwa nguvu za kiume kwa sababu tezidume imevimba, lakini yule kapungukiwa nguvu za kiume kwa sababu misuli ya pelvic floor ni dhaifu; inaingiaje akilini watu wote hao uwape dawa za aina moja na chakula cha aina moja?

Katika kliniki yetu Moro Herbal Clinic tunafanya uchunguzi kwanza, kujua sababu na chanzo kilichosababisha upungufu wa nguvu za kiume. Kisha tunakupangia chakula gani ule na chakula gani usile kulingana na tatizo lako. Kama kuna changamoto ya chakula fulani hakipatikani, basi utatujulisha ili tuweze kubadilisha hicho chakula. Usiendelee kupoteza PESA bure kwa matibabu ya nguvu za kiume yaliyozagaa mitaani yasiyo na tija kabisa.

Pata ushauri bora kabisa kutoka kwa Dr. Abdully, daktari bingwa aliyebobea katika kutibu matatizo ya nguvu za kiume. Anakutibu hadi tatizo lako liishe kabisa. Ni matibabu ya uhakika na wala si ya kubahatisha. Tunakupatia ushauri wa kitaalamu sana wa tiba lishe juu ya tatizo lako la kupungukiwa kwa nguvu za kiume. Na mwisho wa matibabu ni kupona kabisa.

Jinsi tunavyotibu upungufu wa nguvu za kiume kwa chakula

Ndani ya mwili kuna vitu na viungo zaidi ya 100 vinavyoshughulika na nguvu za kiume. Kitu ama kiungo kimojawapo kinapoleta shida nguvu za kiume hupungua. Kuna ubongo, mishipa ya neva ambayo imegawanyika parasympathetic nerve na sympathetic nerve, tezidume (prostate gland), misuli ya pelvic floor, ini, figo, homoni mbalimbali ziko zaidi ya 18 zinazohusika na nguvu za kiume, tezi dundumio, moyo, korodani, uti wa mgongo, n.k. Orodha ni ndefu sana.

Kuna maradhi kadhaa, vyakula tunavyokula, tabia na mtindo wa maisha vinavyoweza kupelekea viungo hivyo kutofanya kazi vizuri. Baaadhi ya maradhi hayo na tabia hizo ni kujichua/punyeto (masturbation); kisukari; presha ya kupanda; presha ya kushuka; uvutaji wa sigara; unywaji wa pombe; madawa ya kuleva; kufanya kazi kupita kiwango na kukosa muda wa kupumuzika; matatizo ya kukosa usingizi na kuchelewa kulala usiku.

Sababu zingine za kupungua nguvu za kiume ni kutokunywa maji ya kutosha, tatizo la kufunga choo hasa pale unapotumia nguvu nyingi kusukuma choo; kutofanya mazoezi; ukosefu wa kumbukumbu; uzito mkubwa/unene mkubwa; kitambi; kuvimba kwa tezidume (Benign Prostate Hyperplasia), n.k.

Sababu zingine ni saratani ya tezi dume (Prostate cancer), matibabu ya mionzi ya tezidume na upasuaji, ugonjwa unaoathiri vitendo na shughuli za mwili kama vile mwondoko na balansi (multiple sclerosis), ugonjwa ambao hudhuru mawasiliano ya ubongo na miondoko ikiwa ni pamoja na kutembea, kuongea na kuandika (parkinson’s disease), vyakula vya mafuta, vyakula vilivyowekewa homoni bandia za kike n.k.

Sababu zingine ni maumivu ya mgongo/kiuno; baadhi ya madhara {side effects} za madawa ya kemikali (madawa ya hospitali); kiharusi (stroke); upungufu katika utendaji wa kazi za gonadi (hypogonadism); uzalishaji mwingi wa homoni ya thyroid

Sababu zingine ni kutozalishwa kwa homoni ya thyroid ya kutosha; ugonjwa unaoathiri uzalishaji wa homoni ya cortisol (cushing’s syndrome); ugonjwa wa kupinda uume (peyronie’s disease); kukakamaa kwa mishipa ya damu (atherosclerosis); orodha ni ndefu sana, ni zaidi ya 200.

Hivyo mwanaume anapopungua nguvu za kiume, ina maana kuna ugonjwa ndani ya mwili wake, au unaweza kuwa huo ugonjwa umeshadhihirika (umeshatokeza) kwa nje, au huo ugonjwa bado uko ndani ya mwili unamla na kummaliza kimyakimya kama yalivyo baadhi ya magonjwa ambapo baadaye hulipuka. Hii ndiyo maana kitaalamu tunasema kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa ni dalili ya ugonjwa. Yani unapopungua nguvu za kiume hiyo ni KENGELE YA TAHADHARI kwamba ndani ya mwili wako kuna kitu au vitu havifanyi kazi vyema. Hivyo, unaambiwa kuchukua haraka  TAHADHARI kabla ya HATARI!

Hakuna dawa moja inayotibu upungufu wa nguvu za kiume kwa wagonjwa wote. Na hakuna ushauri wa chakula wa aina moja kwa wagonjwa wote. Kila mtu na sababu na chanzo chake cha kupungua nguvu za kiume, hivyo kila mtu na dawa yake na ushauri wake wa vyakula. Kuna matibabu ya hovyo kabisa yaliyozagaa mitaani yanayodaiwa kutibu upungufu wa nguvu za kiume. Unakuta mtu kaweka dawa moja kila mtu akija amepungukiwa nguvu za kiume anapewa hiyo dawa. Na huyo anayetibu hata hajui nguvu za kiume ni nini?

Katika kliniki yetu tunapokutibu upungufu wa nguvu za kiume, tunatibu magonjwa yaliyopelekea hali hiyo na tunatibu madhara yaliyoingizwa ndani ya mwili. Tunafanya uchunguzi kujua shida iko wapi. Angalia mfano hapa chini.

Post a Comment

0 Comments