Bawasiri ni nini?
Kabla ya kufahamu dawa sahihi ya asili ya kutibu na kuponyesha kabisa bawasiri, kwanza ni muhimu tufahamu bawasiri ni nini.
Bawasiri ni uvimbe wa mishipa iliyo ndani na karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa au kwenye puru ya chini (puru maana yake kikundu). Bawasiri huathiri mfumo wa mmeng’enyo wa chakula hasa utumbo mkubwa chini mwishoni. Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka ama kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe. Ugonjwa huu unasababisha muwasho na maumivu makali katika tundu la haja kubwa.
Sehemu ya mwisho ya utumbo mkubwa iitwayo anal canal ina urefu wa kiasi cha takribani sentimeta 4. Sehemu ya chini kabisa ya anal canal ni tundu la kutolea kinyesi nje ya mwili (yaani mkundu). Sehemu ya juu yake inaungana na rectum ambayo pia ni sehemu ya utumbo mpana. Anal canal ndio sehemu ya mwisho zaidi ya njia ya chini ya utumbo mkubwa, ambao upo kati ya ukingo wa mkundu (shimo la mkundu) kwenye msamba chini na puru kwa juu.
Kuna mtandao wa veni ndogo (mishipa ya damu) kwenye ngozi inayofunika anal canal. Mara nyingine veni hizi hupanuka na kuruhusu damu nyingi na kuzifanya zitune. Veni hizi zilizotuna na tishu zinazozizunguka zinaweza kutegeneza uvimbe kwenye eneo moja au zaidi, na hii ndiyo huitwa bawasiri, kwa kiingereza piles au pathological hemorrhoids.
Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu unaitwa hemorrhoids jina ambalo limetokana na kuvimba na kuchomoza kwa mishipa ya damu inayopatikana katika puru (rectum) na mlango wa haja kubwa. Na kwa lugha ya Kiingereza unafahamika kama piles. Majina mengine ya bawasiri kwa huku kwetu Tanzania ni Kikundu au Futuri au Puru au Mjiko au Hemoroidi au Mgolo au Mang'ondi.
Matumizi ya kwanza ya neno "hemoroidi" kwa Kiingereza ulitokea mwaka wa 1398, kutoka neno‘’haemoroides’’ kwa Kifaransa, kutoka Kilatini hæmorrhoida -ae", kutoka Kigiriki "αἱμορροΐς" (haimorrhois), "inayoweza kutoa damu", kutoka "αἷμα" (haima), "damu"+ "ῥόος" (rhoos), "mtiririko", kutoka kitenzi "ῥέω" (rheo), "kutiririka".
Kama tulivyoona, bawasiri ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa mkundu ambayo husaidia kudhibiti kinyesi. Katika hali yake ya fiziolojia, hutenda kazi kama mto uliotengenezwa kwa njia ya vena na tishu unganishi. Huwa patholojia (ugonjwa) ikiwa hufungamana kwa kuvimba au kupata inflamesheni.
Mito ya hemoroidi ni sehemu ya anatomi ya kawaida ya binadamu na huwa maradhi pale inapopitia mabadiliko yasiyo ya kawaida. Kuna mito mitatu iliyo katika mfereji wa mkundu wa kawaida. Hii huwa pembeni mwa kushoto, utangulizi wa kulia, na sehemu za nyuma za kulia.
Zimetengenezwa kwa mishipa ya damu inayoitwa sinasi, tishu unganishi na misuli nyororo bali si kwa ateri wala vena. Sinasi haziwi na tishu za misuli katika kuta zao zinazotofautisha kutoka kwa vena zake. Seti hii ya mishipa ya damu huitwa pleksasi ya hemoroidi.
Mito ya hemoroidi ni muhimu kwa ajili ya kushikilia. Huchangia hadi asilimia 15–20% ya shinikizo la kufungika kwa mkundu wakati wa kupumzika na kukinga misuli ya spinkta ya mkundu wakati wa kupitisha kinyesi. Mtu anapoketi chini, presha au shinikizo la ndani la fumbatio huongezeka, na mito ya hemoroidi kuongezeka kwa ukubwa ikisaidia kudumisha kufungika kwa mkundu. Inaaminika kuwa dalili za hemoroidi hutokea wakati miundo hii ya mishipa huteleza upande wa chini au wakati shinikizo la vena linaongezeka sana. Ongezeko la spinkta ya mkundu (presha) shinikizo pia linaweza kuhusishwa katika dalili za hemoroidi.
Bawasiri yaweza kuwa moja ya mada ngumu sana kuzungumziwa kiuwazi na watu. Hii ni kutokana na wagonjwa wengi kuona aibu pengine ni kwa sababu tatizo husika hutokea mahala pa haja kubwa, sehemu ambayo ni ya faragha sana. Wengine huona aibu hata kueleza tatizo hili kwa daktari ama mhudumu wa afya. Ni mojawapo ya matatizo ya kiafya ambayo mara nyingi yanapompata mtu, inakuwa ni ngumu kwenda hospitali ili kupata tiba.
Bawasiri ni tatizo kubwa linawatokea wanaume kwa wanawake. Tatizo la bawasiri huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50% ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 40 mpaka 50. Mara nyingi tatizo hili huwapata watu kuanzia umri wa miaka 25 – 70. Ila kwa sasa ugonjwa huu unawaathiri hata watoto wa umri wa chini kabisa.
0 Comments