Je
wazifahamu siku za hatari kushika mimba? Ni siku gani unaweza kushika mimba
baada ya hedhi kuisha? Mbegu za mwanaume zinaweza kuishi ndani ya kizazi kwa
siku mpaka tano baada ya tendo zikiwa hai. Na mimba inaweza kufanyika endapo
mbegu ipo kwenye kizazi au kwenye mirija ya uzazi wakati yai linatolewa.
Yai kupevuka
Kwa
wanawake wengi yai linapevuka siku ya 14 kwenye mzunguko. Japo kufanya tendo la
ndoa wakati upo period au nyakati zingine ambazo siyo siku ya 14 siyo kigezo
cha kutoshika mimba kwa aslimia mia. Bado mimba inaweza kuingia katika kipindi
kingine mfano ukifanya tendo kipindi cha hedhi.
Je mimba yaweza kuingia kipindi cha hedhi?
Kwa
wanawake wenye mzunguko mfupi yani siku 28 mpaka 30 kuna uwezekano wa kushika mimba hata
ukifanya tendo wakati wa hedhi. Kutumia kinga kama kondomu bado ni njia
ya uhakika zaidi ya kukuepusha kushika mimba usiyoitarajia. Soma zaidi kujua
jinsi ya kupanga siku za kukutana na mme wake ili uepuke kushika mimba
Jinsi Mimba inavyofanyika katika siku za hatari
Yai
linapokomaa hutolewa kwenye mfuko wa mayai(ovary)ili kurutubishwa,kitendo hiki
huitwa ovulation. Kikawaida kila mwezi yai moja hukomaa na kutolewa kwenda
wenye mirija ya uzazi lipate kurutubishwa.
Yai
linakuwa salama masaa 12 mpaka 36 kusubiri mbegu ije irutubishe. Kama mbegu
zinaweza kuishi mpaka siku 5 kwenye kizazi maana yake unaweza ukashika mimba
ukifanya tendo la ndoa kwenye siku za mwisho za hedhi. Siku ambazo
zinakaribiana na siku za yai kupevuka.
Uwezekano
wa kushika mimba unapungua zaidi kadiri siku zinazofuata baada ya siku ya yai
kupevuka. Kama yai lisiporutubishwa ukuta wa kizazi utabomoka na utaanza kuona
damu ikitoka ambayo ndio tunaita hedhi.
Kufatilia siku za hatari kushika mimba kwenye mzunguko
Kufatilia
siku zako za hatari itakusaidia usishike mimba ambapo hujatarajia. Ni zoezi
ambalo laweza kuchukua miezi miwili mpaka mia4 kulifatilia na kulizoea, kwani
yatakiwa kurekodi na kufatilia matukio na mabadiliko yote ya mwili wako.
Unajuaje siku za hatari kushika mimba?
Njia
zifuatazo zitakusaidia kujua siku ya ovulation/siku za hatari
1.Kwa miezi 8 mpaka 12 rekodi siku ambayo unaanza hedhi na
uhesabu siku zote za kila mzunguko. Siku ya kwanza ni ile unayoanza hedhi
katika mwezi husika na hesabu mpaka siku unayoanza hedhi katika mwezi mwingine
hapo mzunguko mmoja utakuwa umekamilika.
2.Rekodi mzunguko mfupi na mzunguko mrefu zaidi katika
ufuatiliaji wako
3.Kupata siku yako ya kwanza ya hatari chukua namba ya
mzunguko mfupi zaidi toa 18, mfano mzunguko wako mfupi ni siku 27-18 inabaki 9.
4.Kupata siku yako ya mwisho ya hatari kwenye mzunguko, chukua siku za
mznguko wakko mrefu toa 11. Mfano mzunguko wako mrefu ilikuwa siku 30-11
inabaki 19.
5.Katika mahesabu hapo juu ni kwamba siku kati ya mzunguko mfupi na
mrefu ndizo siku zako za hatari, kwa maaana ya kuanzia siku ya 9 na 19 ndizo
siku zako za hatari. Kama unataka usishike mimba basi usifanye ngono siku ya 9
ya hedhi mpaka siku ya 19.
Je ni uhakika kiasi gani kutoshika mimba nikifatilia?
Kama
una mzunguko usiovurugika ni rahisi zaidi kufatilia na kuepuka mimba. Fahamu tu
kwamba siku ya ovulation inaweza kubadilika kulingana na mazingira kama stress,
mazoezi, hali ya hewa na lishe.
Njia
hii ya kufatilia siku ni hakika zaidi kama unatafuta mimba. Kwa habari ya
kuzuia mimba uhakika wake unapungua mno. Ongea na daktari akujulishe njia
zingine za hakika zaidi kuzuia mimba na kupanga uzazi.
Njia zingine za kuzuia mimba kwenye siku za hatari
Kuna
njia nyingi za kisasa kuzuia usishike mimba ikiwa hujapangilia.Njia hizi ni
kama
- vidonge vya kuzuia mimba
- kitanzi
- sindano kama depo
- njiti na
- kondomu
- njia hizi ni hakika zaidi kwa
asilimia zaidi ya 90 endapo zikitumika kwa usahihi.
0 Comments